You are currently viewing WASANII HANSON BALIRUNO NA HALIMA NAMAKULA KWENYE KASHFA YA WIZI

WASANII HANSON BALIRUNO NA HALIMA NAMAKULA KWENYE KASHFA YA WIZI

Wasanii Halima Namakula and Hanson Baliruno wameingia kwenye headlines nchini Uganda mara baada ya kutuhumiwa kumtapeli promota wa muziki nchini humo Eddies K Promotions shillling laki 2 za Kenya.

Kulingana na Eddie K Promotions, Halima Namakula na Hanson Baliruno walimuibia pesa hizo baada ya performance yao huko Mubunde nchini Uganda ambapo waliwatishia maisha wafanyikazi wake kwenye gari waliomokuwa wakisafiria na kisha wakatoweka na kiasi hicho cha pesa.

Hata hivyo wawili hao baadae walijitokeza na kukanusha madai ya kumuibia Promota huyo shilling laki 2 kwa kusema kwamba pesa hizo ni malipo ya performance yao lakini Eddie K Promotions amesisitiza kuwa lazima wasanii hao wamerejeshe pesa zake kwa kigezo kuwa hawakustahili kulipwa kiasi hicho cha pesa kwa performance yao mbovu waliyofanya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke