You are currently viewing WASANII UGANDA WAMTAKA BEBE COOL AMSAMEHE BLACK SKIN

WASANII UGANDA WAMTAKA BEBE COOL AMSAMEHE BLACK SKIN

Mtunzi wa nyimbo Black Skin alipelekwa katika gereza la Kitaalya Alhamisi wiki iliyopita kwa mashtaka ya kumlaghai bosi wa Gagamel, Bebe Cool.

Wasanii kadhaa nchini Uganda wamejitokeza na kumtaka Bebe Cool amsamehe msanii huyo kwani wanaweza kutatua tofauti zao bila kuhusisha vyombo vya usalama.

Mwanamuziki Vampino, ambaye ni rafiki wa karibu wa Black Skin ametoa wito kwa Bebe Cool aache suala hilo kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini Uganda.

“Sanaa siku zote ni zawadi, tulitatue hili na tuwe na maelewano katika tasnia yetu ya ubunifu, jela sio suluhisho pekee,” Vampino aliandika kwenye kurusa zake kwenye mitandao ya kijamii.

Wasanii wengine ambao wamemtaka Bebe Cool amuachilie huru wa blacksini  ni pamoja na; prodyuza Eno Beats, Kalifah Aganaga, Pallaso na wengine wengi.

Purukushani kati ya Bebe Cool na Black Skin ilianza pale mwandishi huyo wa nyimbo alipotumia  mitandao ya kijamii kumtuhumu  Bebe Cool  kuwa ameshindwa kulipa deni lake la shillingi elfu 15 za Kenya baada ya kumuandikia wimbo uitwao, “Gyenvude”.

Haikuishi hapo alienda mbali zaidi na kusema kuachia toleo lake la wimbo wa “Gyenvude”, jambo lilimkasirisha Bebe Cool kwani Black Skin pia aliapa kumumaliza Bebe Cool kimuziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke