Wasanii wa Boondocks gang, Exray na Odi wa Murang’a wamejibu tuhuma zilizoibuliwa na aliyekuwa member wa kundi hilo, Edu Maddox.
Wakipiga stori na podcast ya Presenter Ali wasanii hao wamekanusha madai ya kumtumia vibaya Madoxx huku wakisema kwamba msanii huyo alikuwa anapenda sana kuishi maisha ya starehe, kitendo ambacho kilimpelekea kushindwa na shughuli za muziki.
Aidha wamesema kwamba walihamua kujitenga na madoxx kwa sababu alikuwa kizingiti kwa maendeleo ya kundi la Boondocks kimuziki.
Hata hivyo wamepuzilia mbali madai ya kumzuia Maddox kufungua akaunti yake ya youtube kwa kusema kwamba kila msanii wa kundi la Boondocks ana akaunti ya youtube ila uzembe wake wa kutofanya kazi umemfanya kutoachia kazi zake kama msanii wa kujitegemea.
Hata hivyo wamethibitisha kuwa bado kundi la boondocks lipo imara licha ya utofauti ambao mwanachama mwenzao Maddox aliibua kwenye mitandao ya kijamii ambapo wameahidi kumlipia gharama ya kumpeleka rehab.
Kauli ya exray na Odi wa Murang’a inakuja mara baada ya madox kudai kuwa alijiondoa kwenye kundi la Boondocks Gang kwa sababu hakufaidi na chochote kimuziki kutokana na wasanii hao kumtenga kwenye shughuli zao za kimuziki.