Wasanii wa Jeshi Jinga wamemtolea uvivu KRG The Don kwa madai ya kukosoa lugha yao ya Sheng ambayo walibuni hivi majuzi.
Katika mahojiano yao hivi karibuni wasanii hao wamemtaka KRG The Don aache kuwaingilia wakiwa kwenye harakati zao za kuja na lugha mpya itakayowaunganisha watu duniani kwani msanii huyo anatumia suala hilo kutafuta kiki.
Aidha wamesema sheng yao mpya inakidhi vigezo vyote vya kuwa lugha rasmi kwani wamekuwa wakiifanyia kazi lugha hiyo kwa muda mrefu ambapo wamekanusha madai ya kutumia mihadarati kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwa sababu wao ni watu wanajiheshimu sana.
Wasanii hao wameenda mbali na kuwachana baadhi ya wasanii ambao wameanza kutumia lugha hiyo kwa shughuli zao za kisanaa kwa kuwataka waheishimu kama lugha zingine badala ya kutoa nyimbo ambazo hazina mashiko kwenye jamii.
Hata hivyo Jeshi Jinga wamedokeza ujio wa album yao mpya ambayo tayari wameanza kufanyia kazi huku wakiwataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea ngoma yao mpya itakayotoka hivi karibuni.