You are currently viewing WASANII WA KENYA WANG’ARA KWENYE TUZO ZA AEAUSA

WASANII WA KENYA WANG’ARA KWENYE TUZO ZA AEAUSA

Hatimaye mtandao wa tuzo za African Entertainment Awards USA, umetoa majina ya wateule watakaowania tuzo hizo kwa mwaka 2021, huku wasanii chipukizi trio mio na nikita kering  wakiwa miongoni mwa wanaowania tuzo hizo.

Trio Mio na Nikita Kering, katika tuzo hizo wameingia kwenye kipengelea cha msanii Bora chipukizi mwaka wa 2021 ambapo atachuana na wasanii wengine kutoka nchi za Afrika wakiwemo mac voice, Omah Lay, Liya Guchi, Oxlade, na wengine kibao.

Wasanii wengine kutoka Kenya walioingia katika tuzo hizo ni khaligraph jones kupitia kipengele cha msanii bora wa hiphop,sauti sol kupitia kipengele cha kundi bora,  tanasha donna na nadia mukami ambao wameteuliwa kupitia kipengele cha msaniii bora wa kike.

Kipengele cha mchekeshaji Bora Afrika kutoka Kenya kinawakilishwa na Njugush pamoja na Eric Omondi ambaye pia ametajwa kwenye kipengele cha mwanahabari bora wa mwaka.

Pia kipengele cha tuzo Bora ya jukwaa la habari kidijitali kwa Kenya tunawakilishwa na Elsa Majimbo pamoja na Eric Omondi .

Tuzo hizo zilizoanza kutolewa tangu Oktoba 31 mwaka wa 2015, zinatarajiwa kutolewa mapema mwaka wa  2022, nchini Marekani, na tayari zoezi zima la kupiga kura limeanza rasmi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke