Wanamuziki wa Kenya wamepokea mirabaha yao kutoka kwa Chama cha Haki ya watumbuizaji nchini PRISK, iliyopewa mamlaka na bodi ya hakimiliki nchini KCB kuwasimamia kazi za wabunifu wote wanaojihusisha na sanaa.
Kila msanii aliyesajiliwa na PRISK amepokea shillingi 1,215 za kenya kama mapato yake jambo ambalo baadhi ya wasanii wameonekana kupokea shingo upande wakisema kwamba pesa hiyo ni kidogo sana ikilinganishwa na namna muziki unatumika maeneo ya umma na mengine ya burudani.
Mapema mwezi huu Rais Uhuru Kenyatta alitia saini msaada wa marekebisho ya hakimiliki kuwa sheria mpya ambayo inatoa mwongozo ya jinsi wabunifu au wasanii wanapaswa kupokea mgao wa mapato ya kazi zao isiyopungua asilimia 52.