Hatimaye wasanii wa kundi la muziki wa Gengetone nchini Mbuzi Gang wameachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wao.
Mbuzi Gang wamewabarki mashabiki zao na “Three Wise Goats Album” , album ambayo ina jumla ya nyimbo 13 za moto, ikiwa na kolabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, Lava Lava,KRG The Don, Nina Roz,Katapilla, Ethic, Exray Taniua,Madini Classic, Naiboi na wengine kibao.
Album hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Shida, Blessing, Goshodo, Rudi Nyumbani,Shifla, Zoza na nyingine nyingine.
Hii ni Album ya kwanza kwa kundi la Mbuzi Gang ambalo linaundwa na wasanii Fathermoh, Joefes na iphoolish