You are currently viewing WASANII WA KENYA WAMTOLEA POVU ZITO ERIC OMONDI

WASANII WA KENYA WAMTOLEA POVU ZITO ERIC OMONDI

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amejipata pabaya mara ya baada ya wasanii wa muziki nchini kumsuta vikali kwa kauli yake aliyotoa majuzi kuwa muziki wa Kenya umekufa.

Kupitia kurasa zao za instagram wasanii wa Kenya wakiongozwa na Jua Cali wameokana kukasirishwa na kauli hiyo ya Eric Omondi ambapo wamemtaka mchekeshaji huyo akome kuwavunjia heshima wa wasanii wa kenya heshima kwa lengo la kujitakia makuu.

Kauli ya Jua cali imetiwa uzito na Femi one, Bahati pamoja na Bien wa Sauti Sol ambao wamesema Eric Omondi amepoteza dira kwenye kazi zake za ucheshi kwani ameishiwa na mawazo ya kuwashawishi mashabiki zake ndio maana amehamua kuwaingilia wanamuziki wa kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao.

Hata hivyo mashabiki wa muziki nchini wameonekana kutofautia kimawazo na wasanii wanaomshambulia Eric Omondi wakisema kwamba wasanii wa Kenya ndio wameua kiwanda cha muziki kwa sababu hawapeani support kwenye zao muziki jambo ambalo wamedai limepelekea wasanii wa nje kupenya kwenye soko la muziki nchini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke