You are currently viewing WASHINGTON: “NIWADAI WASANII MIRABHA YA SHILLINGI MILLIONI 157”

WASHINGTON: “NIWADAI WASANII MIRABHA YA SHILLINGI MILLIONI 157”

Prodyuza mkongwe wa muziki kutoka uganda David Washngton amedai kuwa anatarajia kukusanya mirabaha ya shillingi million 157 kutoka kwa wasanii aliofanya nao kazi miaka ya hapo nyuma.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema fedha hizo ni kutoka kwa nyimbo zaidi 100 ambazo aliwatayarishia wasanii mbali mbali nchini Uganda.

Washington ambaye amekuwa kwenye muziki kwa takriban mwongo mmoja amesema tayari wasanii kama Cindy Sanyu wameitikia wito wa kuanza kumlipa kwa kazi nzuri aliyowafanyia kwenye muziki.

Hata hivyo Cindy ameapa kumlipa prodyuza huyo mirahaba ya nyimbo zake kwani ni moja kati ya watu ambao walimtambulisha kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Mapema mwezi huu Washington alitoa changamoto kwa wasanii nchini kumlipa mirahaba ya nyimbo ambazo alifanya nao kipindi cha nyuma ambapo aliwataja wasanii kama Bob Wine, Bebe Cool, Cindy Sanyu na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke