You are currently viewing WATU 11 WAFARIKI DUNIA KWENYE TAMASHA LA TRAVIS SCOTT

WATU 11 WAFARIKI DUNIA KWENYE TAMASHA LA TRAVIS SCOTT

Takribani watu 11 wanasadikika kufariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia rabsha zilizotokea wakati wa tamasha la msanii Travis Scott Astro world Fest likiendelea mjini Houston usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, imearifiwa kwamba kuna mtu mmoja miongoni mwa wahudhuriaji wa tamasha la Travis Scott alipagawa na kuanza kuwachoma watu sindano ambayo inadaiwa kuwa na chembechembe za madawa. Kitendo hicho kilizua taharuki kiasi cha kuanza kusukumana ambapo watu takribani 11 wanasadikika kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Baadhi ya waliopoteza maisha wanadaiwa kuwa walipatwa na shambulio la moyo hivyo inahisiwa walidungwa sindano na mtu huyo. Kwa mujibu wa taarifa, inadaiwa kuwa ni shambulio la kupangwa.

Hata hivyo rapa Travis Scott ametoa kauli kufuatia tukio hilo akisema ameshtushwa sana na ametoa salamu za pole kwa familia za wafiwa na wote waliopata majeraha.

Onesho hilo, limeahirishwa. Awali kabla ya onesho kuanza, watu walionekana wakisukumana na kuvunja mageti kutaka kuingia katika uwanja wa NRG Park ambapo tiketi zilikuwa SOLD OUT.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke