You are currently viewing WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

Mwanamuziki kutoka Uganda Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kile kilichotokea kati yake na mfanyikazi wake wa nyumbani ambaye aliripotiwa kupigwa na msanii huyo.

Akiwa kwenye moja ya Interview, Weasel amekanusha kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani huku akisema kwamba alisikia uvumi huo kutoka kwa vyombo vya habari na majukwaa mengine.

Hitmaker huyo wa “Magnetic” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vyombo vya habari vilirusha taarifa hiyo bila kujua kiini cha kupigwa kwa mfanyikazi wake wa nyumbani.

Hata hivyo amesema licha ya mfanyikazi wake wa nyumbani kueleza upande wake wa stori,anasubiri apate nafuu ili aweze kuweka wazi kilichotokea kati yao kwa kina.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke