You are currently viewing WEASEL MANIZO AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI UGANDA

WEASEL MANIZO AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki nchini Uganda Weasel Manizo amewajia juu mapromota wa muziki nchini humo mara baada ya mwanamuziki wa Nigeria Chike kuimba wimbo wake na Mozey Radio uitwao “Breath Away” kwenye moja ya performance yake bila idhini.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Weasel ameonekana kutopendezwa na kitendo hicho huku akiwataka mapromota wa muziki wakome kuwaruhusu wasanii wa kimataifa kuimba nyimbo za wasanii wa ndani bila kuwashirikisha kwani hatua hiyo inashusha ubunifu na brand zao za muziki.

Hata hivyo mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumuunga mkono Weasel Manizo kwa kilio chake hicho kwa kuwataka mapromota wa muziki nchini uganda kuwapa kipau mbele wasanii ndani kwenye shows badala ya wasanii wa kimataifa ambao mara nyingi hushindwa kuwapa mashabiki burudani wanaohitaji.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke