Mwanamuziki Weasel Manizo amefunguka kwa mara ya kwanza baada taarifa za kumshushia kipigo cha mbwa mke wake Sandra Teta kusambaa mtandaoni.
Akizungumzia tukio hilo, Weasel amekanusha vikali tuhuma za kumpiga mke wake kwa kusema kwamba hahitaji msaada wa mtu yeyote katika kuitunza familia yake.
Haikushia hapo ameenda mbali na kusema kwamba ni jambo la kushangaza kuona watu wanamkosoa mtandaoni ilhali wana migogoro katika familia zao.
“Karibu kila familia ina matatizo, mbona unanizungumzia mimi kana kwamba unanijali kuliko mimi? Ninaishi maisha bora na mke wangu na sihitaji msaada wa mtu yeyote katika masuala kama haya. Geuza nguvu zako kwenye mambo mengine,” ameelezea akiwa kwenye moja ya shoo yake usiku wa kuamkia leo.
Duru za kumianika zinadai kuwa wazazi wa Sandra Teta walisafiri kutoka Rwanda hadi Uganda kwa ajili ya kumuokoa binti yao kutokana na manyanyaso aliyokuwa anapitia kwenye ndoa yake.