Mwanamuziki kutoka Uganda Weasel Manizo anajulikuna kuwa ni mtu mwenye hasira sana ameripotiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya aliyekuwa dj wa kundi la Goodlyfe crew dj Triangle kwenye klabu moja ya usiku viungani mwa jiji la Kampala.
Kulingana na chanzo cha karibu na msanii huyo Weasel alianza kumshushia kichapo DJ Triangle baada ya kuingia kwenye ugomvi kabla ya kupata usaidizi kutoka kwa walinzi wake.
Hata hivyo maafisa wa polisi wameanzisha msako wa kumtafuta Weasel ambaye baada ya tukio hilo alisepa na timu yake mafichoni.
Utakumbuka Mwaka jana Weasel alitimukia mafichoni baada ya kumpiga mfanyikazi wake wa nyumbani na kumuacha majeraha mabaya huko Neverland Makindye nchini Uganda.