You are currently viewing WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

WEASEL MANIZZO MBIONI KUJA NA TAMASHA LA KILA MWAKA KUMUENZI MWENDAZAKE MOZEY RADIO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Weasel Manizo ameweka wazi mpango wa kuja na tamasha la kila mwaka kwa ajili ya kumpa heshima marehemu Mozey Radio.

Msanii huyo ambaye alikuwa mwanakikundi wa Goodlyfe Entertainment, amesema tamasha hilo litaitwa Radio Festival na litaanza mapema mwaka wa 2022.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemjia juu baada ya msanii huyo kususia kuhudhuria maombi ya kumkumbuka marehemu Radio wiki iliyopita wakimtaja kuwa mnafiki kwa kushindwa kuendeleza nyayo za mozey radio kwenye tasnia ya muziki nchini  Uganda.

Duru za kuaminika zinasema Weasel Manizo alisusia maombi kutokana na tofauti walizonazo na Familia ya Mozey Radio kuhusu mirabaha ya muziki wa Radio.

Utakumbuka Mozey Radio ambaye alikuwa anaunda kundi la Goodlyfe alifariki mwezi Februari mwaka wa 2018 baada ya kuingia kwenye ugomvi na mlinzi wa night club moja huko Kampala uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke