You are currently viewing WEEZDOM AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAPENZI

WEEZDOM AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAPENZI

Msanii wa muziki nchini Weezdom ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake, amefunguka kwamba ana watoto wanne aliowapata na wanawake tofauti.

Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, mkali huyo wa ngoma ya “Testify” amefunguka mengi kuhusu familia yake kwa kusema kwamba kati ya wanawake wanne aliozaa nao, wawili ni maafisa wa polisi.

Weezdom ameenda mbali zaidi na kuawashauri wanaume ambao wamepata watoto na wanawake tofauti kuhakikisha kwamba wanawapa mahitaji ya msingi watoto waliozaa nao badala ya kuwakimbia.

Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mzima Weezdom kuongelea familia yake,kwani kipindi cha nyuma aliwahi kufunguka kwamba kinachomsukuma kutia bidii maishani ni watoto wake ambao aliwapata na wanawake tofauti.

Ikumbukwe juzi kati Weezdom alithibitisha kuwa yeye na mpenzi wake wa siku nyingi Mylee Staicey sio wapenzi tena,hii ni baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai wawili hao wamerudiana tena.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke