You are currently viewing WEEZDOM AKANUSHA MADAI YA KUFUTWA KAZI NA BAHATI

WEEZDOM AKANUSHA MADAI YA KUFUTWA KAZI NA BAHATI

Msanii wa muziki nchini Weezdom amenyosha maelezo kufuatia post aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram akisema kwamba Bahati akome kufutilia maisha yake.

Akipiga stori na mwana youtube Presenter Ali Weezdom amesema alikasirishwa na kauli ya Bahati kwamba alimfuta kazi kama meneja wake baada ya kuzembea katika majukumu yake.

Msanii huyo amekanusha madai yaliyoibuliwa na bahati kwamba alifuta kazi kama meneja wake kwa kusema madai hayo sio ya kweli kwani yeye binafsi ndiye aliamua kuacha kazi kama meneja wake.

Amesema ameshangazwa na hatua ya Bahati kukosa shukran kwake licha ya kumsaidia mambo mengi kwenye muziki wake ikiwemo kumuandikia wimbo wa barua uliompa mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki.

Weezdom amesema bahati amemfanya aonekane mbaya kwenye jamii kwa kukodisha watu wamtusi kwenye mitandao ya kijamii ambapo amesema hatotishwa na jaribio hilo la kumzima kwani yeye ni moja kati ya watu ambao huwa hajali jinsi watu wanamchukulia.

Hata hivyo amemtaka bahati aache kuwafanyia wasanii wengine mabaya hata kama aliwashika kipindi cha nyuma kwani yeye pia mafanikio ambayo ameyapata yametokana na watu waliomtangulia kumuonyesha njia.

Kauli ya Weezdom imekuja mara baada ya Bahati kunukuliwa kwenye moja ya interview akisema kwamba watu waache kumuuliza kuhusu habari za weezdom ambaye alishindwa kutekeleza majukumu ya kusimamia kazi zake wakati alimpa wadhfa wa umeneja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke