You are currently viewing Weezdom akiri kupatwa na msongo wa mawazo kisa Bahati

Weezdom akiri kupatwa na msongo wa mawazo kisa Bahati

Msanii Weezdom amefunguka kupatwa na msongo wa mawazo baada ya kuachana na aliyekuwa bosi wake chini ya label ya EMB Records, Bahati.

Kwenye mahojiano na Podcast ya EMM, amesema tangu uhusiano wake na Bahati kuingiwa na ukungu, ilikuwa vigumu kwake kujikimu kimaisha jambo lilimpelekea kuchukua maamuzi magumu na kuanza kubugua pombe kupindukia kama njia ya kukimbia changomoto za maisha.

Msanii huyo amesema ulevi ulimfanya kupoteza mweelekeo kiasi cha kusahau kufanya muziki.

Hata hivyo amesema anamshukuru mwenyezi Mungu kwa kumtoa kwenye tatizo la ulevi baada ya wasamaria wema kujitokeza na kumsaidia kuondokana na matumizi ya pombe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke