You are currently viewing WEEZDOM AMJIBU DIANA MARUA BAADA YA KUDAI UBALOZI WAKE NA LIMAVEST NI BANDIA

WEEZDOM AMJIBU DIANA MARUA BAADA YA KUDAI UBALOZI WAKE NA LIMAVEST NI BANDIA

Msanii wa muziki nchini Weezdom amemtolea uvivu mke wa Bahati, Diana Marua baada ya mrembo huyo kupuzilia mbali ubalozi wake na kampuni ya Limavest.

Akipiga stori na mwana youtube presenter Ali, Weezdom amesema kwamba ameshangazwa na kauli ya chuki ambayo diana aliitoa dhidi ya dili alilopewa na kampuni ya Limavest akisisitiza kwamba mrembo huyo ana wivu na mafanikio yake kwani kipindi cha nyuma alinyang’anywa ubalozi wa kampuni hiyo baada ya kukiuka mkataba wa maelewano.

Lakini pia ameeleza kwamba Diana ameiponda dili lake la ubalozi kutokana na hatua yake ya kumkingia kifua Willy Paul kwa tuhuma za uongo alizoziibua dhidi ya msanii huyo.

Hata hivyo amesema ubalozi wake na kampuni ya Limavest ni halali na sio feki kama jinsi ambavyo Diana Marua amewaaminisha watu kwenye mitandao ya kijamii.

Kauli ya Weezdom imekuja mara baada ya Diana Marua kudai kuwa taarifa za Weezdom kulamba dili la ubalozi  wa kampuni ya Limavest ni za uongo kwani msanii huyo anatumia jina la kampuni hiyo kutengeneza kiki ili azungumziwe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke