You are currently viewing WEEZDOM AMVUA NGUO EX WAKE MYLEE STACY KWA KUMPOROMOSHEA MATUSI MAZITO

WEEZDOM AMVUA NGUO EX WAKE MYLEE STACY KWA KUMPOROMOSHEA MATUSI MAZITO

Aliyekuwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Weezdom ameingia tena kwenye Headline kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumporomoshea Matusi Ex wake Mylee Stacy kwa hatua ya kuivuruga ndoa yake.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Weezdom ameonekana kukasirishwa na kitendo cha Ex wake huyo kumtumia jumbe za mapenzi nyakati za usiku akiwa na mke wake ambapo ameenda mbali zaidi na kumtaka Mlyee Stacy akome kumpigia mke wake simu kila mara na badala ya akubali kwamba mahusiano yao yalivunja kitambo.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahisha na kitendo cha weezdom kumtolea mambo mazito ex wake Mylee Stacy ambapo wamemshauri wangetatua tofauti zao nje ya mitandao ya kijamii kwani wanajiahibisha wenyewe.

Utakumbukwa Weezdom na Mylee Stacy wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda ambapo wamekuwa wakiachana na kurudiana lakini uhusiano wao uliingiwa na ukungu mwishoni mwaka wa 2020 baada ya Stacy kudaiwa kutoka kimapenzi na dancer wa FBI aitwaye Ezra madai ambayo  mrembo huyo alikuja akakanusha vikali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke