You are currently viewing WEMA SEPETU AKANUSHA KUITISHA MICHANGO YA KUNUNUA GARI

WEMA SEPETU AKANUSHA KUITISHA MICHANGO YA KUNUNUA GARI

Msanii wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu amesema kuwa hajawahi kuwatuma watu kukusanya michango kwa ajili ya kununua gari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam , Wema amesema aliona jambo hilo na kuwaambia wasitishe kwa sababu hakuridhika nalo na hakumtuma mtu kufanya hivyo.

“Mimi binafsi sikuwahi kumwambia mtu yeyote anichangie pesa, nadhani ilikuwa ni upendo na watu wakaamua wafanye hicho wanachofanya lakini nilishawaambia siko comfortable, na wasitishe na nina imani walishitisja,” amesema.

“So, sijui nini kilitokea baada ya hapo na sikutaka kujihusisha toka mwanzo kwa sababu sijawahi kumuomba mtu michango ya gari” amesema Wema Sepetu.

Utakumbuka jambo hilo lilibuka mara baada ya Mjasiriamali maarufu mtandaoni, Aristote kumshambulia Wema kwa madai hana gari zuri la kifahari kama ilivyo kwa Irene Uwoya, kauli iliyopokelewa kwa hisia kali na wengi hadi Aristote mwenyewe kuomba radhi

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke