You are currently viewing WEMA SEPETU ANYOSHA MAELEZO KUFANYA MUZIKI WA BONGOFLEVA

WEMA SEPETU ANYOSHA MAELEZO KUFANYA MUZIKI WA BONGOFLEVA

Muigizaji maarufu Bongo Movie, Wema Sepetu ameweka wazi kuwa hana mpango wa kujitosa kwenye muziki.

Mrembo huyo, amebainisha kuwa ana uwezo wa kuingiza sauti yake kwenye nyimbo za wasanii wengine.

“Mimi huwa napenda kuingiza zile sauti za nyuma, kuimba siwezi, sitaki kujitia aibu, kama wasanii wanapenda sauti zile za nyuma, mimi niko vizuri Hamna wimbo wowote wa Wema unakuja,” amesema.

“Sitegemei kuingia kwenye kuimba kwa kweli. Mtanicheka nikianza kuimba, siko tayari,” alisema Wema akiongea na Wanahabari juzi kati.

Hata hivyo amefichua kuwa amewahi kuingiza sauti yake kwenye nyimbo kadhaa za aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz, kama Lala Salama na Chanda Chema

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke