WhatsApp imeweka mabadiliko kwa kuweka uwezo wa kuzuia mtu asiweze kupiga screenshot katika picha au video ambayo mtu ametuma kwa kutumia option ya “View Once”. Lakini pia inazuia mtu asiweze ku-screen record!
Mabadiliko haya yameanza rasmi na kwa watumiaji wote ambao wanatumia toleo jipya (updated) app. Mtu akipiga screenshot au kurekodi screen picha haionekana na anapewa ujumbe kuwa WhatsApp imezuia screenshot/screen-record.
Ikumbukwe bado watu wataweza kutumia simu nyingine kurekodi au kupiga picha hivyo sio mabadiliko ambayo yanaweka uhakika na usalama.