You are currently viewing WHATSAPP KUWEKA MFUMO WA KUPOKEA NA KUTUMA CRYPTO

WHATSAPP KUWEKA MFUMO WA KUPOKEA NA KUTUMA CRYPTO

Miezi sita iliyopita kampuni ya Meta ilitoa Wallet yake ya Crypto ambayo inaitwa Novi Wallet na inatumia Stablecoin ya Pax Dollars (USDP) ambayo ni crypto yenye thamani sawa na Dola 1.

WhatsApp imeanza majaribio ya kuunganisha Wallet ya Novi na WhatsApp hivyo utaweza kutuma na kupokea pesa moja kwa moja katika WhatsApp kwa kuunganisha Wallet ya Novi na app yako ya WhatsApp.

Majaribio hayo yameanza kwa watumiaji wa Marekani ikiwa ni sehemu ya kujaribu mfumo na kucheck utaratibu wa kupata vibali na kupima mfumo. Mfumo wa WhatsApp hauna makato katika mihamala.

Apps nyingi zinapambana kuweka urahisi huo ili kutangulia mbele katika ulimwengu wa malipo ya mitandao na umiliki wa fedha za kidigitali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke