You are currently viewing WHATSAPP KUWEKA UWEZO WA KUTENGENEZA STICKERS

WHATSAPP KUWEKA UWEZO WA KUTENGENEZA STICKERS

WhatsApp inaweka uwezo wa kutengeneza stickers katika app ya Android na iOS; na pia katika WhatsApp PC na WhatsApp Web.

Watumiaji wa WhatsApp watakuwa na uwezo wa kutengeneza stickers moja kwa moja katika app ya WhatsApp. Hii itapunguza usumbufu wa kutumia app za kutengeneza stickers ambazo nyingine zimekuwa zikihitaji subscriptions na charges za kupata premium stickers.

Ukifungua app ya WhatsApp, sehemu ya attachments, mbele ya stickers utaona option ya ku-upload picha na tools za kutengeneza sticker kupitia picha ambayo umeweka. Unaweza kuongeza texts, michoro na emoji katika stickers.

Tayari mabadiliko yameanza katika WhatsApp Web, wiki chache zifuatazo itawekwa kwa watumiaji wa Android na iOS.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke