You are currently viewing WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

App ya WhatsApp inafanya majaribio ya kuweka mfumo mpya wa “Voice Message au Notes”. Mfumo huo mpya utawezesha watumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message hata ukiwa umefunga chat na kufungua chat nyingine au kurudi kwenye list ya messages.
 
Kwa kawaida ukiwa unasikiliza Voice Message katika WhatsApp, ukiifunga chat na Voice Message inaacha kucheza, hivyo inabidi ubaki katika chat ikiwa unataka kusikiliza Voice Message. Mfumo mpya wa Voice Messages utawezesha mtumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message huku akiwa amefungua chat nyingine tofauti na chat ambayo Voice Message imetumwa.
 
Kwa juu itakwepo line ya rangi ambayo inafanana na Audio Player ambapo mtumiaji atakuwa na uwezo wa ku-pause, Play na kufunga Voice Message. Lakini pia  voice note hiyo itakuwa na uwezo wa kuonyesha jina na profile ya chat ambayo imetuma Voice Message.  Itasaidia endapo kama kuna chats nyingine ambazo inakubidi ufungue kwani utakuwa na uwezo wa kuendelea na shughuli nyingine katika app hiyo huku ukisikiliza Voice Message kwa pamoja.
 
Feature hii ipo katika majaribio katika mfumo wa iOS, na itatoka kabla ya mwaka huu kuisha. Ni mabadiliko ambayo tayari yapo Telegram kwa muda mrefu sana.
 
 
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke