WhatsApp imepata kibali cha kuongeza watumiaji Milioni 40 katika service yake ya WhatsApp Pay nchini India.
Hapo awali, WhatsApp ilikuwa na kibali cha kuwa na watumiaji Milioni 20 hivyo kwa sasa ina limit ya watumiaji Milioni 60.
Bado WhatsApp Pay ipo katika sehemu ya majaribio nchini Brazil na India. Ni sehemu ya mfumo ambao utawezesha watumiaji kutuma na kupokea fedha katika app ya WhatsApp.
Pia watumiaji watakuwa na uhuru wa kulipa bidhaa na kutumia katika WhatsApp Business.