You are currently viewing WHATSAPP YAWEKA MFUMO WA DISAPPEARING MESSAGES KATIKA CHAT ZOTE

WHATSAPP YAWEKA MFUMO WA DISAPPEARING MESSAGES KATIKA CHAT ZOTE

Wiki hii WhatsApp inaweka uwezo wa kuchagua mfumo wa Disappearing Messages katika chats zote mpya. Disappearing Messages ni option ya kuamua chats zifutike baada ya masaa 24, Siku 7 au Siku 90.

Mfumo mpya unaofanana na mfumo wa Snapchat, utawezesha watumiaji kuweka option ya Disappering Messages katika chats zote mpya. Mwanzo ilikuwa unaweka option hii kwa mtu mmoja mmoja.

Meta imesema sababu ya kuweka hivyo ni kuwapa watu uhuru wa kuepuka ku-save messages nyingi hasa wale ambao wanapata messages nyingi za watu wapya na hakuna umuhimu wa kutunza chats.

Bado ni option, mtu anaweza kuamua kuzima au kuweka option hii.

Kwa watumiaji wa Android na iOS, feature hii itakwepo katika WhatsApp Settings > Account > Privacy > Default Message Timer. Hakikisha ume-update WhatsApp yako katika App Store au Google Playstore.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke