You are currently viewing Whozu afunguka kuhusu mimba ya Wema Sepetu

Whozu afunguka kuhusu mimba ya Wema Sepetu

Mwimbaji wa Bongofleva, Whozu amethibitisha kuwa ni kweli alimpa mimba mpenzi wake Wema Sepetu ila ikaharibika.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, Whozu amebainisha kuwa kuharibika kwa ujauzito wa Wema ilikuwa bahati mbaya.

Mwanamuziki huyo ameeleza kusikitishwa kwake na watu waliotilia shaka habari za yeye kumpachika mimba mpenziwe.

“Iliniuma, halafu watu wanafikiria ni uwongo! Mnanionaje kuwa mimi siwezi kumpa mtu mimba? Mnanichukuliaje?,” alisema.

Whozu amedokeza kuwa anapanga kumpa Wema ujauzito kwa mara nyingine baada ya ule wa kwanza kutofikia hatua ya kujifungua.

“Lazima niweke pale, lazima kuwa na Lola na mdogo wake Lola. Naomba Mungu awe wa kiume, mama yake atakuwa Wema Sepetu,” alisema.

Hata hivyo amesema kuwa bado anafanya juhudi nyingi na pia anamuombea sana mpenzi wake apate ujauzito tena.

Haya yalijiri baada ya Wema Sepetu kueleza hamu yake ya kupata mtoto wa kwake na kumuomba Mungu amjalie.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke