Hatimaye Mwigizaji Will Smith hatoruhusiwa kuhudhuria Tuzo za Oscar kwa miaka 10 kutoka sasa ikiwa ni adhabu baada ya kumpiga kibao Mchekeshaji Chris Rock jukwaani wakati wa Tuzo hizo za mwaka huu.
Smith hatoruhusiwa kuhudhuria hafla au programu zozote za Academy, yeye binafsi au hata kwa mtandao.
Lakini pia barua hiyo imeeleza shukrani nyingi kwa Chris Rock kwa utulivu wake wakati wa hali isiyo ya kawaida.
Hata hivyo, baada ya marufuku hii ya miaka 10 Will Smith ameonesha kukubali adhabu aliyopewa kwa kuiambia CNN kwamba anakubali na kuheshimu uamuzi huo.