Mwiigizaji na mwanamuziki kutoka Marekani Will Smith ametawala vichwa vya habari duniani asubuhi hii baada ya kumshushia kichapo mchekeshaji Chris Rock live Jukwaani wakati wa ugawaji wa Tuzo za Oscars.
Chris Rock alifanya utani juu ya mke wa Will Smith, Jada Pinkett ndipo Will Smith aliamka na kupanda Jukwaani ambapo alimchapa kofi la nguvu mchekeshaji huyo na kumwambia mara mbili “Keep my wife’s name out of your f-cking mouth.”
Baadaye Will Smith alipanda Jukwaani baada ya kushinda Tuzo ya Best Actor ambapo kwenye hotuba yake alisema alifanya kitendo hicho kwa lengo la kulinda familia yake dhidi ya chochote.
Hata hivyo aliishia kuomba radhi mbele ya wahudhuriaji na kila mmoja aliyekuwa akitazama tuzo za Oscar kupitia runinga.