You are currently viewing WILL SMITH AZINDUA KITABU KIPYA KUHUSU MAISHA YAKE

WILL SMITH AZINDUA KITABU KIPYA KUHUSU MAISHA YAKE

Mwanamuziki,Muigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Marekani, Will Smith amezindua kitabu chake kipya kipya kiitwacho “Will” ambacho kinaangazia maisha yake

Kwenye kitabu hicho ambacho kilizinduliwa rasmi  Novemba 9, mwaka huu, Will Smith amesimulia kuhusu maisha yake kama mtu maarufu na maisha yake binafsi.

Will smith amesimulia kuhusu uhusiano kati yake na baba yake mzazi ambao anasema haukuwa mzuri.Lakini pia amefichua kwamba amewahi kujaribu kujitoa uhai mara mbili maishani na mara ya kwanza alijiwa na wazo hilo akiwa na umri wa miaka 13 wakati mama yake mzazi aliondoka nyumbani.

Jambo jingine ambalo Smith amezungumzia ni urafiki kati ya mke wake Jada na rapa Tupac Shakur. Jada na Tupac walilelewa eneo moja na pia walifanikiwa kwenda chuo pamoja katika chuo cha sanaa kinachofahamika kama “Baltimore School for the Arts”.

“Mwanzo wa uhusiano wangu wa kimapenzi na Jada, urafiki wake ya Tupac ulinitishia, uliamsha woga ndani yangu kwa sababu alikuwa nyota mkubwa na mimi sikuwa ninajulikana.” – Will Smith.

Kitabu chicho chenye jumla ya kurasa 432 kinapatikana kwenye majukwaa kadhaa ya kuuza vitabu mitandaoni na kinapatikana pia kwa sauti ambayo ni ya Will Smith mwenyewe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke