You are currently viewing WILLIS RABURU ATOA YA MOYONI KUHUSU WASANII WANAOTUMIA KIKI KUTANGAZA VITUO VYA AFYA

WILLIS RABURU ATOA YA MOYONI KUHUSU WASANII WANAOTUMIA KIKI KUTANGAZA VITUO VYA AFYA

Hitmaker wa ngoma ya “Kalale”, Msanii Willis Raburu amewatolea uvivu mastaa wa muziki nchini ambao wamekuwa  na mazoea ya kuwahadaa Wakenya kupitia kiki za kufeki Magonjwa.

Kupitia waraka mrefu aliouchapisha kwenye mitandao yake ya kijamii Willis ameonesha kukerwa na tabia ya baadhi ya mastaa kufeki magonjwa kwa ajili ya kuzitangaza huduma za vituo vya Afya.

Willis ambaye ni mwaandishi wa habari katika runinga ya Citizen Kenya amewakosoa mastaa hao kwa kukosa ubunifu huku akisema kuwa sio lazima waigize kuwa wagonjwa kutangaza huduma za hospitali wazoingia ubia wa kufanya kazi nao kwani sio kitendo cha kingwana.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii wa muziki nchini kuwa wangalifu wanapokuwa wanatangaza biashara za makampuni ili wasiwape wafuasi wao taswira mbaya kuhusu matangazo husika.

Kauli ya Willis Raburu imekuja mara baada ya msanii wa nyimbo za injili nchini Size 8 kuwashangaza wakenya kwenye mitandao ya kijamii aliposhare video clip akiwa amelazwa hospitalini ambapo alienda mbali na kudai kuwa anaumwa na kusindikiza na caption ya jina la hospitali hiyo.

Kitendo hicho kiliibua ukakasi miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi walihoji kuwa msanii huyo hakuwa mgonjwa  ila alikuwa anazitangaza huduma ambazo hospitali hiyo inatoa kwa wateja wak

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke