Mwanamuziki maarufu nchini Willy paul amewataka mashabiki zake kuacha kumuita jina la utani la Mkunaji.
Kupitia instagram Willy paul amesema jina hilo ni la kishetani na lina mikosi mingi, hivyo hataki kuhusishwa nalo.
Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema tangu aanze kutumia jina la mkunaji amejipata kwenye kashfa nyingi ambazo amedai zimemuaharibia chapa au brand yake ya muziki.
Hata hivyo amewaomba mashabiki zake kuacha kumuita mkunaji huku akisema kuwa imelazimika kuairisha suala la kuachia video ya wimbo wake wa toto kwa ajili ya kuhakikisha jina hilo linaondolewa kwenye video ya wimbo huo.
“Morning fam, would like to take this opportunity to let everyone know that from today hence forth I will not be using the name ” MKUNAJI ” it’s evil and I don’t want to be associated with it! Ever since I embraced the name I’ve had too much problems. So if you’re truly a fan of Willy Paul, Willy Pozze. Stop calling him ” MKUNAJI ” We’re postponing the release of #TOTO video just to do away with this name, to make sure that it’s nowhere.
You’ll notice afew changes when the #toto video drops. 2022 is not a year of problems!”..ameandika willy paul kupitia instagram page yake.