You are currently viewing WILLY PAUL ACHUKIZWA NA WASANII WA KENYA KUMKIMBIA KWENYE BIRTHDAY

WILLY PAUL ACHUKIZWA NA WASANII WA KENYA KUMKIMBIA KWENYE BIRTHDAY

Hitmaker wa “Tamu Walahi”, Msanii Willy Paul amesikitishwa na hatua ya wasanii wenzake kutomuonyesha upendo wakati wa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake juzi kati.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul ameposti video akiwa na mashabiki zake ambapo amesema alitarajia wasanii wenzake wamtakia heri ya siku ya kuzaliwa lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja ambaye alisimama naye kwenye siku yake hiyo muhimu.

Hata hivyo amewashukuru mashabiki pamoja na baby mama wake kwa upendo ambao walimuonyesha kwenye birthday yake huku akisema amefarajika sana na salamu zao za heri.

“This are my fans!! They surprised me today, I must say I’m very humbled by this action…. I expected some people that i share alot with to atleast wish me a happy birthday… but non of them did… I’m glad my daughters mother wished me a happy one!! Love you all and thank you for making my sad birthday a happy one… bless you!.” Ameandika kwa uchungu.

Willy Paul ambaye alitimiza umri wa miaka 29 Septemba 2 mwaka huu, kwa sasa yupo mbioni kuwabariki mashabiki zake na album yake ya tatu iitwayo Not Thing But Love ambayo kwa mujibu wake huenda ikaingia sokoni mwakani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke