You are currently viewing WILLY PAUL ADATA NA SHEPU YA SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI AMBER RAY

WILLY PAUL ADATA NA SHEPU YA SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI AMBER RAY

Mwanamuziki Nyota nchini, Willy Paul ameweka wazi kuzimia umbo la Mwanasosholaiti maarufu nchini, Amber Ray.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya “Toto” amepost picha ya pamoja akiwa na Amber Ray na kusema kwamba mrembo huyo hajafanya upasuaji wowote kuongeza sehemu yoyote ya mwili wake kama wanavyofanya akina dada wengi kwa sasa.

“Hiyo nguo imepiga kona, chochote unachoona kwake ni real,” amendika Willy Paul Insta.

Ujumbe huo umetafsiriwa kuwa ni vijembe kwa msanii Niccah The Queen ambaye juzi kati amerushiana maneno makali na Amber Ray kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya Nicah kudai kuwa Amber Ray amekuwa na mazoea ya kutoka kimapenzi na waume wa watu.

Utakumbuka Willy Paul amekuwa akimsifia Amber Ray katika siku za hivi karibuni kupitia mitandao yake kijamii ikiashiria kuwa huenda mrembo huyo ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Willy Paul kama Video Queen.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke