You are currently viewing Willy Paul afikisha subscribers milioni 1 Youtube

Willy Paul afikisha subscribers milioni 1 Youtube

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amefanikiwa kufikisha idadi ya subscribers million moja kwenye mtandao wa Youtube

Channel ya youtube ya Willy Paul ilifunguliwa rasmi Mei 21 mwaka 2010 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 193,063,998.

Willy Paul sasa anajiunga na wanamuziki wenzake Otile Brown na Bahati ambao wana zaidi ya wafuatiliaji (subscribers) Milioni 1 kwenye mtandao Youtube nchini Kenya.

Bosi huyo wa Saldido amepata mafanikio hayo mara baada ya video ya wimbo wake “Lalala” aliyomshirikisha Jovial kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube kwa madai ya hakimiliki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke