You are currently viewing WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUJA NA MUONEKANO MPYA

WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUJA NA MUONEKANO MPYA

Mionekano kwa wasanii si jambo la kuchukulia poa, bali ni kazi. Ni moja ya njia za branding na kujiweka machoni mwa mashabiki muda wote.

Msanii nyota nchini Willy Paul amefunguka sababu za kunyoa nywele zake aina ya dreadlocks wiki iliyopita.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Willy Paul amesema kuwa ameamua kuja na muonekano mpya kwa sababu ameacha kabisa miendo yake ya zamani ambayo amedai kuwa yalimletea matatizo kwenye safari yake ya muziki.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Chocolate” ameweka wazi sababu ya ukimya wake kwenye mitandao ya kijamii akisema kwamba kuna project ambayo anaifanyia kazi kwa sasa hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke