Staa wa muziki nchini Willy Paul amefunguka sababu za kutoachia wimbo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki kati yake na msanii wa Nigeria Guchi.
Kwenye mahojiano na Mungai Eve Willy Paul amesema video ya ngoma hiyo ilivuja mtandaoni, kitendo ambacho kilimkasirisha na kuamua kufutilia mbali mchakato wa kuachia wimbo huo.
Lakini pia ameweka wazi chanzo cha kufuta video ya wimbo wake wa “Moyo” kwenye mtandao wa Youtube kwa kusema kuwa video ya wimbo huo haikuwa na ubora aliouhitaji, hivyo aliogopa itamshushia chapa au brand yake ya muziki.
Willy paul ambaye amegonga vichwa vya habari kwa wiki moja sasa baada ya kuwekeza kwenye sekta ya matatu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Kesho.