Msanii Willy Paul a ameamua kutoa ya moyoni kuhusu namna madalali wamekuwa kizingiti kwa wasanii kupenya kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya.
Kupitia instastory amesema amesikitishwa na namna wasanii wasiokuwa na vipaji wanapewa kipaumbele kwenye matamasha ya muziki huku wasanii wanaotoa muziki mzuri wakiambulia patupu.
Amesema kenya ina wasanii wengi ambao wanafanya vizuri kimuziki lakini wamenyimwa nafasi ya kuonyesha dunia kazi zao kutokana na madalali ambao wamevamia tasnia ya muziki kuwazingatia wasanii wasiokuwa na vipaji.
Hata hivyo ametaka tasnia ya muziki nchini kufanyiwa maboresho kwa kuwaondoa wasanii wanaolemaza juhudi za wasanii walio na vipaji kutanua wigo wa muziki ili uweze kuwafikia watu wengi duniani.
Hata hivyo hajajulikana ni kitu gani hasa kilimpelekea msanii huyo kuzungumza jambo hilo ila baadhi ya watu wanahisi huenda amenyimwa nafasi ya kutumbuiza kwenye moja ya matamasha ya muziki nchini.