Staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza hataachia album yake mpya iitwayo “The African Experience” kama ilivyokuwa imepangwa.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amesema hatua ya kuahirisha kutoka kwa album hiyo ni fursa nzuri kwake kujiandaa vilivyo na kuwapa mashabiki wake kazi nzuri.
Hata hivyo, bosi huyo wa Saldido records hajasema album hiyo itatoka lini na ni mabadiliko yapi anayafanya.
African Experience album ambayo ilipaswa kutoka oktoba 22 ikiwa ni exclusive kwenye jukwaa la boomplay, ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na Kelly Khumalo