You are currently viewing WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amekanusha madai ya kuiba idea ya wimbo wake mpya uitwao “Atoti Jaber” kutoka kwa msanii mwenzake Ringtone Apoko.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul amemtaka Ringtone akome kueneza taarifa za uongo kwamba alimuibia wimbo wa “Atoti Jaber” huku akisema madai hayo hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa wimbo huo aliomshirikisha Klons Melody na Jakadalla sio wimbo wa injili.

Those of you that know Ringtone know the kind of person he is.. My brother please stop telling your friends that I stole the song atotijaber from you. It has never been a gospel song, enough with your clout chasing bro. It’s 2022, new beginnings. I love and respect you as a big brother who came to this industry before me.

To all my fans, keep supporting the song #atotijaber x @klons_melody x @musajakadalla_ ameandika Willy Paul kupitia Instagram yake

Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema amechoshwa na sarakasi za Ringtone ambapo ameenda mbali na kumtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutangaza kazi zake za muziki badala ya kutengeneza mitukio ili azungumziwe na vyombo vya habari nchini.

Hata hivyo amesema anamheshimu Ringtone kama mmoja wa wasanii waliomtangulia kwenye tasnia ya muziki huku akiwataka mashabiki waendelee kusapoti wimbo wake wa “Atoti Jaber” kwenye digital platflorms mbali mbali za muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke