You are currently viewing WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

Msanii nyota nchini Willy Paul ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake,amefunguka kwamba alipitia kipindi kigumu mara baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kingono aliyekuwa msanii wake Miss P.

Kwenye mahojiano na Munga Eve, Hitmaker huyo wa “Tamu Walahi” amedai kuwa tuhuma hizo ziliathiri afya yake ya akili kiasi cha kupatwa na msongo wa mawazo huku akiri kuwa tangu kipindi hicho hajawahi kurejea katika hali yake ya kawaida kwani amekuwa akiishi kwa hofu.

Katika hatua nyingine amesema hatokuja kumsaini msanii yeyote kwenye lebo ya Saldido kwa kuwa wasanii aliowasajili kipindi cha nyuma walimshushia tuhuma za uongo ambazo karibu zimuharibie chapa yake ya muziki.

Utakumbuka mwishoni mwa mwaka jana kipindi Miss P anaondoka kwenye lebo ya Saldido alimtuhumu Willy Paul kumdhulumu kijinsia kiasi cha kumlazimisha kutoka nae kimapenzi bila kutumia kinga.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke