You are currently viewing WILLY PAUL AMALIZA BIFU YAKE NA ERIC OMONDI

WILLY PAUL AMALIZA BIFU YAKE NA ERIC OMONDI

Hatimaye staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza kumaliza bifu yake na mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi baada ya wawili hao kurushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kwa muda.

Kupitia ukurasa wake wa instagram willy paul amemtaka Eric Omondi kuwa waache matukio yasioyokuwa na msingi na badala yake waupambanie muziki wa kenya uweze kusikilizwa zaidi kimataifa.

Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema bifu kwenye muziki hazisaidii kwani zinarudisha tasnia ya muziki nchini ambapo amemtakia Eric Omondi kila la kheri kwenye harakati za kuupambania muziki wa Kenya.

Ikumbukwe bifu kati ya Willy Paul na Eric Omondi ilianza wakati mchekeshaji huyo alimshauri bosi huyo wa Saldido kubadilisha jina la msaani wake mpya Queen P huku akisisitiza kuwa Miss P ambaye alikuwa msanii wa Willy Paul atasalia kuwa mmoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke