Nyota wa muziki nchini Willy Paul amemtolea uvivu mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi kwa madai ya kumlinganisha msanii wake mpya Queen P na aliyekuwa msanii wake Miss P.
Kupitia instastory yake Willy Paul amemtaka Omondi akome kufuatilia maisha yake na badala yake ajishughulishe na mambo ambayo yatamuingizia kipato.
Ikumbukwe juzi kati Willy Paul alimtambulisha Queen P kama msanii wake mpya ndani ya lebo ya muziki ya Saldido International ikiwa ni miezi kadhaa tangu waachane na aliyekuwa msanii wake Miss P ambaye anasimamiwa na Eric Omondi.
Willy Paul tayari ameachia singo yake mpya iitwayo “Pressure” aliyomshirikisha msanii wake Queen P ambayo inazidi ya views laki moja tangu itoke Novemba 21.