You are currently viewing WILLY PAUL AMTAKA BAHATI AACHE SIASA

WILLY PAUL AMTAKA BAHATI AACHE SIASA

Msanii nyota nchini Willy Paul inaonekana hajafurahishwa namna ambavyo msanii mwenzake Bahati anavyohangaishwa kwenye azma yake ya kuwa mbunge Mathare.

Hii ni baada ya Bahati kurushiana maneno makali na Katibu Mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna kwenye mtandao wa Twitter baada ya muungano wa Azimio la Umoja kumtangaza Anthony Olouch kuwa mgombea wao kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.

Kupitia mtandao wa twitter Willy Paul amenshauri Bahati  aachane kabisa na masuala ya siasa na badala yake arudi kwenye uimbaji waendelezee harakati zao za kuupeleka muziki wa kenya kimataifa.

Kauli hiyo ya Willy Paul imeshabikiwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakionekana kumtaka Bahati ajiondoe kwenye siasa kwa sababu hatawezana nayo kwa kuwa ni jambo linalohitaji ujasiri mkubwa.

Haya yanajiri wakati huu Bahati ameingia kwenye ugomvi na muungano wa Azimio la Umoja baada ya muungano kumtaka ajiuzulu kwenye azma yake ya kuwa Mbunge mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na badala yake aungu mkono azma ya mbunge wa sasa Mathare Anthony Oluoch ambaye anatetea kiti chake kwa mara ya pili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke