Nyota wa muziki nchini Willy Paul amemtambulisha msanii mwingine wa kike, miezi kadhaa baada ya kuondoka kwa msanii wake wa kwanza Miss P.
Kupitia ukurasa wake wa instagram willy paul amesema msanii huyo kwa jina la Queen P atakuwa chini ya lebo ya saldido ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ambapo amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini.
Kusainiwa kwa Queen P kumekuja miezi kadhaa baada ya aliyekuwa msanii wake wa kwanza Miss P kudai kuwa willy paul alidhulumu kimapenzi akiwa chini ya lebo yake.
Novemba 12 mwaka huu, Pozze alishare nasi nyaraka za mahakama zilizomtaka Presenter Ali kufuta mahojiano yake na Miss P ambaye alidai kwamba msanii huyo alimnyanyasa kingono mara kadhaa.
Nyaraka hizo zilieleza kuwa yeyote atakayeeneza au kusambaza video hiyo atachuliwa hatua kali za kisheria kwa madai ya kumhariba willy paul jina.
Ikumbukwe mwezi Mei mwaka huu, Willy Paul alimtabulisha msanii mwingine wa kiume kwenye lebo yake aitwaye Klons Kenya lakini msanii huyo hajaonekana kwa muda, na haijulikani kama bado yupo chini ya lebo hiyo au aliondoka.