You are currently viewing WILLY PAUL AMVUA NGUO DIANA B KUPITIA “NIKOME” DISS-TRACK

WILLY PAUL AMVUA NGUO DIANA B KUPITIA “NIKOME” DISS-TRACK

Inaonekana bifu la Msanii Willy Paul kwa mke wa Bahati, Diana B linaelekea pabaya na halitapoa hivi karibuni. Hii ni baada ya Willy Paul kuachia disstrack iitwayo “Mnikome” ambapo amemvua nguo Bahati na mke wake Diana B.

Kwenye diss track hiyo Willy Paul moja ya mistari ambayo imeibua hisia mseto miongoni mwa wadau wa muziki nchini ni ile amesikika akimtaka bahati afanye vipimo vya dna kwa watoto aliozaa na mke wake diana kwani kuna uwezekano mkubwa watoto hao sio wake.

Hata hivyo Bahati na mke wake Diana B hajatoa tamko lolote kuhusiana na diss track hiyo ila ni jambo la kusubiriwa.

Ikumbukwe bifu la Willy Paul kwa familia ya Bahati ilianza baada ya mke wa Bahati, Diana B kudai kwamba Willy Paul anamuonea wivu kwenye kazi zake za muziki kwa sababu amemshinda kwa idadi ya views kwenye mtandao wa Youtube.

Hii imekuja mara baada ya Willy Paul kudai Bahati amemnunulia mke wake views youtube kwani nyimbo zake mbili “Hatutaachana” na “One Day” zimefanikiwa kufikisha zaidi ya views millioni moja ndani ya kipindi kifupi, kitu ambacho hakijakuwa kikifanyika kwa wasanii wa Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke