You are currently viewing WILLY PAUL AMVUA NGUO SANAIPEI TANDE

WILLY PAUL AMVUA NGUO SANAIPEI TANDE

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amemtolea povu zito msanii Sanaipei Tande baada ya mrembo huyo kuzuzia kushiriki kwenye album yake ijayo iitwaýo The African Experience.

Sanaipei alidinda kufanya collabo na Willy Paul kwa sababu msanii huyo ana skendo nyingi lakini pia anapenda sana kujihusisha na masuala ya kiki kitu ambacho anadai kuwa hakipendi.

Sasa Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul ameonekana kusikitishwa na matamshi ya sanaipei kwa kusema kwamba hakutarajia msanii huyo anaweza toa kauli kama hiyo ikizingatiwa kuwa alitaka kufanya nae collabo kwa sababu ni moja kati ya watu ambao walimu-inspire kimuziki.

Pozze ameenda mbali zaidi na kujinasibu kwamba ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kumliko Sanaipei Tande lakini hawajawahi kuwa na kiburi kama ya Sanaipei Tande huku akisema kuwa hajawahi mkosoa msanii huyo kwa njia yeyote ile.

Hitmaker huyo “Diana” amesema Sanaipei Tande amekosa fursa kubwa katika maisha yake ya muziki kwa kudinda kuwa mmoja wa wasanii watakaoshiriki kwenye Album yake mpya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke