You are currently viewing WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

Staa wa muziki nchini Willy Paul hatimaye ameiomba radhi familia ya Bahati baada ya kupewa makataa ya saa 24 kufanya hivyo la sivyo atafunguliwa mashtaka kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Diana Marua.

Willy Paul awali alidai kuwa miaka kadhaa iliyopita alitoka  kimapenzi na mke wa Bahati japo hakubaka kama namna ambavyo Diana Marua alimtuhumu.

Sasa kupitia screenshot ya ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii willy paul ameonekana akimlilia Bahati amsamehe kutokana na kile kinachoendelea mtandao.

Sanjari na hilo Willy Paul amemtumia Bahati Barua akisema kwamba madai yake ya kutoka kimapenzi na mke wake Diana Marua sio ya kweli kwani kiki tu,  hivyo Bahati anapaswa kuelewa kwani ni sehemu ya matukio ambayo utokea kwenye tasnia ya muziki.

Hata hivyo haIjabainika kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo ikizingatiwa kuwa Willy Paul wala Bahati hajatoa tamko lolote.

Utakumbuka Januari 13 mwaka huu kuna barua ilikuwa inasambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya wakili wa Diana Marua ambapo kwenye barua Willy Paul alipewa makataa ya saa 24 aombe msamaha la sivyo afungulie kesi mahakamani kwa madai ya kumharibia jina diana marua kuwa aliwahi toka nae kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke